Njiwa aliyesafiri katika bahari ya Pacific amewasilli Australia wakati ambao kuna sheria kali za kutotoka nje.
Ndege huyo aliripotiwa kupotea wakati wa mashindano huko Oregon, Marekani mwishoni mwa mwezi Oktoba, na akaonekana miezi miwili baadae katika mji wa Melbourne .
Lakini maofisa wanasema njiwa huyo, ambaye amepewa jina la Joe, anaweza kuwa na maambukizi na kuhatarisha ndege wa Australia.
Ndege huyo atakamatwa na kuuliwa.
Mkazi wa Melbourne Kevin Celli-Bird anasema walimkuta ndege huyo nyuma ya bustani Desemba 26.
"Alionekana kuwa na njaa kali hivyo nilimpelekea biskuti ," aliliambia shirika la habari la AP.
Baadhi ya utafiti wa intaneti ulioongozwa na bwana Celli-kugundua ndege huyo ambaye aliandikishwa kwa mmiliki wa Alabama, alionekana mara ya mwisho katika mashindano ya njiwa huko magharibi ya jimbo la Oregon nchini Marekani.
Lakini baada ya taarifa za kupotea kwa Joe kuwa kwenye vichwa vya habari nchini Australia, bwana Celli-Bird aliwasiliana na mamlaka kuhusu wasiwasi wake wa tishio la maambukizi.
Njiwa huyo alikuwa hajakamatwa bado lakini idara ya kilimo,maji na mazingira inasema auawe kwa sababu anaweza kuambukiza ndege wengine.
"Kutokana na uasilia wake,ndege yeyote wa ndani hajakutana naye na hajapimwa afya yake bado ya kumfanya kubaki nchini Australia," msemaji wa idara alisema.
"Suala ambalo linawezekana kufanyika ili kudhibiti hatari ya maambukizi ni kumuua ndege huyo."
Haijawekwa wazi ndege huyo amewezaje kusafiri maili 8,000-kutoka fukwe za Marekani mpaka Australia, lakini maafisa wanaamini kwa labda alikuja na mizigo.
Ingawa inawezekana kufika kihalali kwa ndege huyo nchini Australia, ingawa utaratibu wake huwa ni mgumu unaweza kugharimu fedha nyingi kumsafirisha kutoka Marekani kihalali na inaweza kuchukua hata zaidi ya muongo.
Joe sio mnyama wa kwanza kukutana na wakati mgumu Australia kwasababu ya sheria kali za kusafirisha wanyama.
Muigizaji Johnny Depp na mke wake Amber walionekana kwenye video wakiomba radhi kwa mbwa wao Pistol na Boo kuingia nchini humo kinyume na sheria kwa kutumia ndege binafsi mwaka 2015.