"Bad Friends Virus" Kirusi Kinachotafuna Wanawake Wengi Duniani


Moja kati ya vitu ambavyo vinawatafuna wanawake wengi kutokufika katika kilele cha mafanikio ni marafiki. Katika kundi la wanawake kumi basi nane huwa na marafiki wa ovyo na wawili ndio huwa na marafiki sahihi. Kwa lugha nyengine mwanamke ndio muathirika namba moja wa (Bad friend virus)


Hasara za kuwa na rafiki mbaya katika maisha ni kubwa sana kuliko tudhaniavyo. Rafiki mbaya anaweza kukusababishia kupoteza matumaini ya maisha yako kwa kukuambukiza tabia hatarishi zenye madhara maishani. Rafiki mbaya anaweza kukusababishia ukaonekana mtu mbaya kwa watu kumbe kosa la rafiki yako.


Bad friend virus ni kirusi kinachotafuna watu wengi katika dunia ya sasa bila wenyewe kujijua. Rafiki anatakiwa kuwa msaada kwako hata kwa hali kama hakuna mali. Rafiki anaekuhamasisha mnunue sale za kusutia wakati nyumba wanayolala wazazi wako paa lake mbingu, huyo ni 'Bad friend virus' haraka jitenge nae.


Rafiki mwenye jini kudanga hana haja ya kazi nyengine yoyote zaidi ya kudanga, huyo ni 'Bad friend virus' vaa maski uwepo nae karibu kabla hajakuua. Thamani ya mwanamke ni kubwa kiasi cha kutotosheleza kuelezea. Andika kila rafiki na faida yake kwenye daftari lako kisha anza kukata mmoja mmoja ambae huoni faida ya kuwa nae.


Kupunguza aina za marafiki wa ovyo kwako kutastawisha maisha yako na kutakuweka mbali na hatari ya kupata virusi hivi vibaya vya 'Bad friend virus'. Lazima mwanamke uwe msimamizi wa maisha yako ili kwa faida yako na kizazi chako. Amua leo kujitenga na Bad friend virus.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad