Biden: Marufuku raia wa Afrika kusini kuingia Marekani




Baada ya kukosolewa kwamba lengo lake la asili halikuwa na nguvu ya kutosha , Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia Marekanu hivi karibuni itaweza kuchanja watu milioni 1.5 kwa siku.



Alikuwa ametangaza wiki iliyopita kwamba chanjo milioni 1 zitatolewa kila siku katika siku 100 za kwanza za urais wake.

Lakini vyombo vingine vya habari vilibainisha kuwa Marekani tayari ilikuwa karibu kufikia lengo hilo chini ya utawala wa Trump.

Bwana Biden ameweka upya marufuku ya enzi ya Trump kuhusu marufuku ya kusafiri kutokana na janga la corona siku ya Jumatatu, akiiongeza Afrika Kusini.

Utawala wa Biden Jumatatu uliweka upya marufuku ya kusafiri ya enzi ya Trump kwa wageni ambao sio Wamarekani kutoka Brazil na na nchi nyingi za Ulaya , pamoja na Uingereza na Ireland.

White House pia imeweka marufuku mpya kwa Afrika Kusini kutokana na uwepo wa virusi aina mpya nchini humo Rais wa zamani Donald Trump aliamuru marufuku kuisha tarehe 26 mwezi Januari.

Masharti mapya ya kusafiri yamekuja wakati Minnesota ikirekodi maambukizi ya mtu mmoja ya kirusi kipya cha Brazil ambaye hivi karibuni alisafiri kwenda nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad