Bobi Wine asema kufungwa kwa Intaneti kulivuga uchaguzi




Bobi Wine amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini intaneti na mitandao ya kijamii vilifungwa kama njia ya kuvuruga kura.
Mgombea wa upinzani tayari amedai kuwa kulikuwa na wizi na mawakala wake pamoja na wawakilishi wameendelea kukamatwa.

Lakini mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Simon Byabakama, amesema kuwa Bobi Wine ana jukumu la kutoa ushahidi kwamba kuna wizi.

Amesema kuwa wagombea walikuwa na mawakala ambao walishuhudia kuhesabiwa kwa kura katika vituo vya kukusanya na kuhesabu kura.

Ni vituo viwili tu vya upigaji kura vilivyoripoti dosari za shughuli za kupiga kura zikasitishwa katika vituo hivyo.

Katika kituo kimoja cha kupigia kura, mtu mmoja alitoroka na sanduku la kura.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kufungwa kwa intaneti ni hatua sahihi na muhimu iliyochukuliwa kuimarisha
    na kuiweka nchi katika hali ya Usalama na Amani.

    Madhara yake kama ingekuwa hewani nikma yaliojiri kwa mwenzenu Till lampu.

    Utalaumu kila kitu mpaka mama watoto, Rudi kufanya kolabo na Nguli wa Hip Hop One and Only HAMORAPA the Great on his new Album.

    Uongozi mwachie General Yoweri Kaguta Museveni ( BABA LAO )

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad