Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema yuko tayari kufanya kazi na rais mpya wa Marekani Joe Biden katika malengo yao ya pamoja ikiwemo kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri Mkuu Johnson ameyasema hayo hapo jana baada ya kuzungumza na Biden kwa njia ya simu. Amekaribisha pia hatua ya Marekani kujiunga tena na makubaliano ya Paris ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kulingana na msemaji wa Boris Johnson, Ili kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Uingereza na Marekani juu ya masuala ya usalama na ulinzi, viongozi hao wawili wamejitolea kuendelea kuukumbatia muungano wa NATO na kuendeleza maadili ya pamoja katika kuunga mkono haki za binaadamu na kulinda demokrasia.