WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Sylvestre Ilunga Ilunkamba, amejiuzulu rasmi wadhifa huo na kuwasilisha barua yake kwa Rais Félix Tshisekedi.
Ilunga, ambaye ni mshirika mkuu wa mtangulizi wa Rais Tshisekedi, Joseph Kabila, ameongoza baraza la mawaziri la Serikali ya Muungano kwa miezi 15.
Hata hivyo, wabunge walipitisha kura ya kutokuwa na imani na serikali yake Jumatano wiki hii na akapewa saa 24 awe amejiuzulu. Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Tshisekedi kuwateua washirika wake kama mawaziri.
Hadi sasa, utendaji wa Tshisekedi umekuwa ukidhibitiwa na muungano alionao na Kabila ambao uliafikiwa wakati alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Ushindi wake katika uchaguzi mwezi Desemba 2018 ulisifiwa kama wa kihistoria, ambapo kulikuwa na makabidhiano ya kwanza ya utawala kwa njia ya amani ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika historia ya miongo sita nchini humo. Tshisekedi bado hajamchagua waziri mkuu mpya ambaye ataunda serikali ijayo.
L