Burundi yafunga mipaka yake baada ya kuongezeka kwa wagonjwa wa corona






Burundi imetangaza kufunga mipaka yake ya ardhi na majini kufuatia ongezeko kubwa la watu waliopatikana na virusi vya corona.
Watu100 wamepatwa na maambukizi mpaya ya virusi vya corona nchini Burundi, ikiwa ndio itadi kubwa ya maambukizi kuwahi kushuhudiwa tangu ugonjwa huo ulipoibuka mwezi machi 2019.

Kuanzia leo Jumanne hakuna mtu yeyote atakayeweza kuvuka kuingia au kutoka nchini Burundi isipokuwa kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa ndege pekee.

Katika mji mkuu Bujumbura imeanzishwa kampeni ya kupima virusi vya coronaImage caption: Katika mji mkuu Bujumbura imeanzishwa kampeni ya kupima virusi vya corona

Hata hivyo wasafiri watakaoingia kwa ndege nchini humo watalazimika kwenda moja kwa moja katika hoteli maalumu na kuishi huko kwa siku saba amkako watapimwa virusi vya corona.

Aidha serikali imetangaza kuanzisha shughuli ya upimaji wa virusi vya corona kwa wakazi wa mji mkuu Bujumbura kwa yeyote anayehisi kuwa ana dalili za Covid-19.

Tayari watu zadi ya 980 wamekwishapatwa na virusi vya corona nchini Burundi na watu wawili ndio waliokufa kwa virusi hivyo kulingana na takwimu za wizara ya afya ya Burundi
OP

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad