Bweni Lililochomwa Moto 2018 Laungua Tena, Kura zapigwa Kubaini Mhusika

 



Sehemu ya bweni la wavulana wa shule ya sekondari Mang'oto wilayani Makete Mkoani Njombe,imeungua moto na kusababisha hasara ya baadhi ya vifaa vilivyokuwemo katika bweni hilo.


Mkuu wa wilaya ya Makete Veronika kessy ametembelea katika shule hiyo na kusikitishwa na tukio hilo ikizingatiwa kuwa bweni hilo liliwahi kuungua kwa kuchomwa moto na mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo mwaka 2018 na ameagiza  kuchukuliwa hatua mara moja.


“Nilipopokea taarifa za kuungua kwa bweni la Mang’oto.nimepatwa na mfadhaiko kwasababu bweni hili liliungua mwaka 2018 mwezi wa 3 na tukafanya jitihada kubwa kuchangisha wananchi,wadau ili kuweza kutoa fedha na kurudisha hili bweni sehemu yake,sasa katika kipindi cha miaka miwili bweni linaungua tena katika mazingira yale yale”alisema Veronika kessy


Kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na maafisa wengine wa serikali wamefika katika shule hiyo ambapo  katika hatua za awali limendeshwa zoezi la kupiga kura ili kuwabaini wahusika na baada ya zoezi hilo kamati hiyo imeondoka na wanafunzi kadhaa kwa mahojiano zaidi.


Mkuu wa wilaya ya Makete Veronika Kessy amesema hatua hizo ni za awali huku akiwataka wanafunzi wanaowafahamu waliofanya kitendo hicho kutoa ushirikiano kupitia kwa walimu wao.


“Kama kuna mtu mnamfahamu amefanya hicho kitendo mumfuate mwalimu wa malezi nenda ukamwambie,itakuweka huru”Dc Kessy aliwaeleza wanafunzi


Afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu Gift Kyando amewaeleza wanafunzi kutambua wajibu wao wawapo shuleni.


“Ukasirike vyovyote lakini sio kuchoma bweni wala kuchoma darasa,ninyi mmechoma bweni mara ya pili sasa,wazazi wenu huko wanahangaika wewe unachoma mahala pa kulala”aliwaeleza wanafunzi mwalimu Gift Kyando


Afisa elimu wa kata hiyo Furaha Kyando  amemteua mwalimu Jacob Mdibwa kusimamia shule kwa kipindi ambacho uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad