RASMI Klabu ya Chelsea imemtambulisha Thomas Tuchel kuwa mrithi wa mikoba ya Frank Lampard ambaye amechimbishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo mbovu.
Kocha huyo ameanza kazi rasmi ndani ya Stamford Bridge kwa ajili ya kuwanoa wachezaji ambao walikuwa chini ya Lampard.
Lampard alifutwa kazi Januari 25 kabla hajapewa mkataba wa kuwa kocha mkuu ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England na aliiacha ikiwa nafasi ya 9 ikiwa na pointi 29.
Tuchel amejiunga na Chelsea akiwa huru baada ya kufutwa kazi ndani ya Klabu ya PSG inayoshiriki Ligue 1 ambayo kwa sasa ipo chini ya Mauricio Pochettino aliyefutwa kazi ndani ya Tottenham Hotspur.
Kocha huyo amesaini dili la mwaka mmoja na nusu na una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja mbele ikiwa atafanya kazi kwa umakini na kuipa matokeo timu yake.
Tuchel amesema kuwa anafurahi kupata kazi ndani ya kikosi hicho huku akiahidi kuonyesha ushirikiano kwa wafanyakazi wote.
"Ninafurahi kuwa hapa na nina amini nitaonyesha ushirikiano ndani ya timu, pia ninaheshimu ambacho amekifanya Lampard kwa kuwa amefanya jambo kubwa na kazi yake ni nzuri," .