Lokosa aliachana Esperance ya Tunisia hivi karibuni lakini Chikwende amenunuliwa kutoka FC Platinum ya Zimbabwe ambayo ilitolewa na Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
SHINDA ZAWADI YA SIMU KWA KUDOWNLOAD APPP YA UDAKU SPECIAL HAPA
Mwanaspoti limejiridhisha kwamba Lokosa na Chikwende walitua Dar es Salaam juzi na jana walimalizana na Simba kabla dirisha dogo halijafungwa. Mnigeria huyo ambaye alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Nigeria msimu wa 2018 amesajiliwa kuongeza nguvu kwenye hatua ya makundi Afrika.
Lokota jezi yake ilitarajiwa kutengenezwa jana usiku, lakini Chikwende amepewa namba 4 iliyokuwa inavaliwa na Taddeo Lwanga ambaye atabadilishiwa.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba usajili wa Chikwende unamaanisha Mkenya Francis Kahata atatolewa kwenye kikosi cha ligi ya ndani na majukumu yake yatakuwa ni kimataifa tu mpaka mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu.
Habari zinasema kwamba Simba ilipanga kumpeleka kwa mkopo Azam FC, lakini jamaa akagoma na kutaka kusalia Msimbazi au mkataba wake uvunje apewe mkwanja wake alale mbele.
Habari zinasema kwamba Simba waliafikiana kwamba asalie Msimbazi ili kukwepa gharama na Chikwende usajili wake umegharimu Sh127milioni na rasmi ametambulishwa jana usiku saa 5:59.
Habari zinasema kwamba Simba walifikiria kumpiga chini Bernard Morrison lakini gharama yake ya kulipa fidia ya mkataba wa mwaka mmoja ni ndefu. Katika hatua nyingine Azam Fc walikuwa wakihusishwa na Chikwende lakini jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema walikuwa na mpango wa kumsajili ila kocha akamkataa.