CHINA imepiga marufu watu kutotoka nje katika maeneo ya kitongoji kimoja katika mji wake mkuu wa Beijing, ikiwa ni kupambana na janga baya zaidi la kuibuka tena kwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Katika vita vya kupambana na ugonjwa huo ambavyo vimeikumba nchi hiyo kwa miaka sita, vijiji vyote katika wilaya ya Shunyi vilivyo kaskazini-mashariki kwa Beijing, watu zaidi ya milioni 1.2 wamefungiwa katika makazi yao huku serikali ikifanya juhudi za kupambana na virusi hivyo.
Wakazi wa maeneo hayo wamepigwa marufuku kutoka nje hadi wakithibitika kuwa hawajakumbwa na ugonjwa huo.
Katika kaunti ya Wangkui yenye wakazi wapatao 440,000 katika Mkoa wa Heilongjiang kaskazini-mashariki kwa China, watu hawatakiwi kutoka katika makazi yao baada watu 20 kuhisiwa kukumbwa na ugonjwa huo, japokuwa hawakuonyesha dalili.
Kuibuka kwa janga hilo kumeilazimisha China kupiga marufuku wakazi wa miji mikubwa kusini mwa nchi hiyo, kusimamisha usafiri sehemu mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wimbi la kuibuka kwa ugonjwa huo huko Shijiazhuang, jiji la mamilioni ya wakazi katika mkoa wa Hebei ambapo vitongoji vyake vina wakazi milioni 11.
Maambukizi pia yamegunduliwa katika jiji jirani la Xingtai ambapo lina wakazi milioni saba.
Habari hizo zinakuja baada ya kupita mwaka mmoja tangu China ilipothibitisha kifo cha kwanza kutokana na virusi ambavyo wakati huo havikutambulika huko Wuhan. Katika kipindi hicho, virusi hivyo hadi sasa vimeua watu wapatao milioni 1.9 duniani.
Katika siku za karibuni, China ilionekana kuudhibiti ugonjwa huo ambapo wananchi wake walianza kurejea katika maisha yao ya kawaida, lakini katika wiki moja iliyopita ugonjwa huo umeibuka katika Jimbo la Hebei eneo la Beijing.