Takukuru Mkoa wa Mara imekamata jumla ya maboksi 40 ya dawa za binadamu zilizokwisha muda wake wa matumizi, katika hospitali za serikali na vituo vya afya binafsi mkoani humo, huku wakiwashikilia watu wawili kwa tuhuma za ugawaji wa dawa hizo.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara, Alex Kuhanda.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Alex Kuhanda, amesema kuwa dawa hizo zilizomaliza muda wake zina thamani ya milioni 56.
“Kitu ambacho hatuna uhakika nacho kama hawa wanaogawa haya madawa, wanawagawia na ndugu zao au hawawagawii lakini ni madawa ambayo yameisha muda wake, na tumewakamata watu wawili na wako ne kwa dhamana”, amesema Kuhanda.
Katika hatua nyingine Kuhanda amesema wameanza kutoa huduma ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kupata malalamiko na taarifa za rushwa