Baada ya akaunti yake ya @realDonaldTrump kufungwa kabisa, Trump alituma ujumbe kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani @Potus akisema kuwa “ataangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wao utakaowezesha mawasiliano siku za usoni” na kukosoa Twitter.
Hata hivyo, ujumbe wake ulifutwa katika jukwaa hilo la mawasiliano muda mfupi baada ya kuwekwa.
Donald Trump's tweets from @POTUS account, 8 January 2021
Akijibu baada ya kupigwa marufuku, mshauri wa kampeni ya Trump 2020 Jason Miller ameandika kwenye Twitter “Inachukiza… ikiwa hujafikiria kwamba wewe ndio wa pili watakaekufuata, umekosea.”
Kwanini Twitter ulikuwa mtandao maarufu sana kwa Trump?
Bwana Trump alitumia mtandao wa Twitter kutukana wapinzani wake, kushabikia washirika wake, kuwafuta kazi maafisa, kukanusha “taarifa za uongo” na kutoa malalamishi yake, mara nyingi akiandika kwa kutumia herufi kubwa na alama za mshangao kusisitizia anachozungumzia.
Ingawa wakosoaji wake wamesema mara nyingi ujumbe wake ulikuwa wa kupotosha, mtandao huo ulimsaidia kukabiliana na mengi na mara moja angefanikiwa kuwasiliana na wafuasi wake karibu milioni 89.
Pia ujumbe wake mara kadhaa ulikuwa na makosa ya herufi na wakati mwingine aliacha wafuasi wake kukisia tu kile alichomaanisha.
Idara ya sheria ilisema mwaka 2017 kuwa ujumbe wa Bwana Trump ulikuwa “mawasiliano rasmi ya Rais wa Marekani”.