Kiongozi Mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameweka ujumbe mtandaoni akitoa wito Donald Trump ashambuliwe kama hatua ya kulipiza kisasi mauaji ya komanda wa juu wa jeshi, Jenerali wa kikosi maalum cha Iran Qasem Soleimani.
Picha kwenye tovuti yake rasmi inamuonesha aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump akicheza gofu katika kivuli cha ndege ya kivita au ndege kubwa isiyo na rubani.
Mtandao wa Twitter umefunga akaunti ambayo ilikuwa ya kwanza kuweka picha hiyo.
Msemaji wa mtandao huo amezungumza na shirika la Reuters na kusema akaunti hiyo – @khamenei_site – ilikuwa ni feki na ilikiuka kanuni za mtandao wa Twitter.
Hata hivyo, ujumbe huo ulitumwa tena na Ayatollah Khamenei katika akaunti ya Twitter kwa lugha ya Farsi yenye wafuasi zaidi ya 300,000. Na tangu wakati huo haionekani tena.
Ruka Twitter ujumbe, 1
#Iran : The threatening tweet against #Trump WAS retweeted on Ayatollah Khamenei’s main Farsi twitter account – not just the odd small one now removed Here is the screengrab It’s now been removed This surely raises questions about the main Farsi twitter site pic.twitter.com/DZf96X6iFu
— sebastian usher (@sebusher) January 22, 2021
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
1px transparent line
Katika ujumbe huo wa Twitter ulioandikwa kwa lugha ya Farsi, neno “kulipiza kisasi” limewekwa kwa rangi nyekundu huku ujumbe mwingine ukisema: “Muuaji wa Soleimani na aliyeagiza kutekelezwa kwa mauaji hayo lazima watalipa”.
Katika mtandao rasmi wa Ayatollah Khamenei, picha hiyo imewekwa na kuoneshwa kuwa muhimu. Na maneno yaliofuata ni matamshi yake aliyotoa Desemba 16, akiahidi tena kulipiza kisasi “muda wowote ule”.
Mtandao wa Twitter uliombwa kuchukua hatua baada ya watumiaji kuchukulia hilo kama upendeleo wakidai kuwa Bwana Trump alifungiwa kutotumia mtandao huo, mbona isiwe vivyo hivyo kwa kiongozi huyo wa Iran.
Mtandao wa Twitter ulifunga akaunti ya Trump iliyokuwa na ushawishi mkubwa mapema mwezi huu baada ya yeye kuweka ujumbe ulioshawishi uvamizi na bunge la Marekani.
“Inawezekanaje huyu mnafiki anaweza kutoa wito wa mauaji ya aliyekuwa rais wa Marekani tena wazi kabisa na asifungiwe kutumia mtandao wa Twitter?”, Mtumiaji mmoja aliandika kwa Kiingereza.
“Trump alipigwa marufuku lakini huyu anaachwa tu. Bila shaka huu ni utani sio, au?”, Mtumiaji mwingine aliandika.
Ujumbe wa Twitter wa Iran ulirejelea Jenerali Soleimani, aliyeuawa kwa kutumia ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani Baghdad mwaka mmoja uliopita.
Chini ya uongozi wa Soleimani, Iran ilikuwa imeimarisha makundi ya wanamgambo wanaopendelea Iran, akaongeza uwepo wake wa kijeshi nchini Iraq na Syria na kutekeleza mashambulizi nchini Syria dhidi ya makundi ya waasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa muda mrefu.
Gen Soleimani alikuwa maarufu sana nchini Iran
Bwana Trump wakati huo alisema jenerali huyo “alihusika ama moja kwa moja au kwa njia isiyo moja kwa moja kwa mauaji ya mamilioni ya wat
Iran ilijubu kwa kurusha makombora kadhaa katika kambi ya wanajeshi nchini Iraqi iliyokuwa ni makazi kwa wanajeshi wa Marekani na kuonya kutekeleza mashambulizi zaidi, huku Ayatollah Khamenei wakati huo akisema “wahalifu wasubiri tukio kubwa la kulipiza kisasi”.
Twitter ilipiga marufuku ujumbe kutoka kwa Ayatollah mapema mwezi huu uliokuwa unaelezea chanjo za virusi vya corona zilizotengenezwa Uingereza na Marekani kama “zisizoaminika”.