Hamu na wepesi wa kutaka 'kushare' picha za Mtoto wako kwenye Mitandao ya Kijamii na Blogu hauzuiliki kirahisi. Kwa bahati mbaya, athari za maamuzi hayo nazo haziepukiki
Licha ya kwamba imekuwa ni kitu cha kawaida kuweka picha za Watoto mitandaoni, zipo athari ambazo zinaweza kumkuta Mtoto ikiwemo picha hizo kuibwa na kutumiwa na Watu baki au wenye nia ovu
Mara nyingi picha zinazopigwa kwa simu huonesha mahali ulipo (GPS) au ambapo picha ilipigwa. Hii inaweza kumfanya Mtu akajua mahali ulipo au sehemu Mtoto wako anaposoma na kuweza kumdhuru
Kuweka picha za utupu ama mtoto akioga. Swali la kujiuliza ni iwapo Mtoto wako akizikuta picha za namna hii miaka 10 au 20 baadaye zitamletea furaha/fedheha pale zitakapoonwa na marafiki zake au watu anaofahamiana nao?