Mojawapo ya mambo muhimu licha ya hali unayopambana nayo kama Mjamzito ni ambavyo unalala hasa katika miezi 3 ya mwisho ya ujauzito. Unaweza kulala kwa upande wako wa kulia na kushoto lakini chali?…hapana na hata usithubutu
Kulala chali kunasababisha mshipa mkubwa wa Damu uliopo tumboni mwa Mama kufinywa kutokana na uzito wa Mtoto na hivyo kumnyima Mtoto Oksijeni ya kutosha. Wanasayansi walifanya utafiti kuhusu hili kwa Wajawazito 1,760 kutoka Uingereza, New Zealand na Australia
Madaktari wanashauri Wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto, kwasababu Mjamzito anapolalia ubavu wa kushoto huongeza mzunguko wa Damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.