MABOSI wa Yanga ambao ni wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya GSM wapo katika mazungumzo ya mwisho kwa ajili ya kuwaleta hapa nchini Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Enyimba SC ya Nigeria.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Simba iliyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya klabu hiyo, bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ wazilete hapa nchini TP Mazembe ya DR Congo na Al Hilal ya Sudan.
Simba imezileta timu hizo katika michuano maalum waliyoiandaa iliyopewa jina la Simba Super Cup inayotarajiwa kuanza kesho Jumatano jijini Dar.
Spoti Xtra, linafahamu kuwa wiki ijayo Yanga itaileta timu moja kati ya Mamelod Sundowns au Enyimba kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafi ki utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
“Katika kuhakikisha Wanayanga wanapata burudani nzuri, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na GSM wamepanga kuileta moja ya klabu kubwa hapa nchini itakayokuja kucheza mchezo wa kirafi ki wa kimataifa.“
Lengo likiwa ni kuwapima wachezaji wao na kingine kuwangetengezea mechi fi tinesi iliyopotea baada ya ligi kusimama katika kipindi hiki kupisha michuano ya CHAN.
“Pia mchezo huo watautumia kuwatambulisha wachezaji wao wapya ambao ni Fiston (Abdoul Razack) na Job (Dickson) waliosajiliwa katika dirisha dogo lililofungwa wiki iliyopita,” alisema mtoa taarifa huyo.
Yanga, jana iliingia kambini kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.