Baraza la Mitihani nchini (NECTA) limetangaza matokeo ya kitaifa ya upimaji wa maarifa kwa darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne kwa mitihani iliyofanyika mwaka jana, 2020.
Akitangaza matokeo hayo jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.09 ikilinganishwa na yale ya kidato cha nne kwa mwaka 2019.
Aidha, Msonde amesema kuwa baraza hilo limefuta matokeo ya watahaniwa 215 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.