Hizi ndio takwimu kuelekea Manchester Derby

 


Manchester United wanawaalika majirani zao Manchester City kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Carabao CUP leo Usiku, ikiwa ni katika harakati za kusaka tiketi ya kucheza fainali katika dimba la Wembley, na mshindi wa mchezo huo atacheza dhidi ya Tottenham kwenye mchezo wa fainali.


Manchester United wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na mwenendo mzuri wa matokeo kwani hawajapoteza mchezo hata 1 kwenye michezo yao 10 ya mwisho, lakini pia wanashuka dimbani leo usiku wakiwa hawajarusu bao kwenye michezo ya raundi 3 zilizopita kwenye michuano hii, huku wao wakiwa wamefunga mabao 8, na wamezitoa timu za Luton Town, Brighton & Hove Albion na Everton.


Kwenye raundi 3 zilizopita Manchester City wameitoa AFC Bournemouth, Burnley na Arsenal, na vijana wa Pep Guardiola waliuanza msimu taratibu, lakini kwa sasa taratibu wameanza kurejea kwenye ubora wao na wameshinda michezo yao yote 4 ya mwisho ukiwemo ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka England.


Timu hizi zilishakutana kwenye mchezo 1 wa ligi kuu na timu hizo zilitoka suluhu, hii ni mara ya 4 timu hizi zinakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe hili la ligi,  zimewahi kukutana msimu wa 1969-70, 2009-10 na 2019-20.


Manchester United wataikosa huduma ya mshambuliaji Edinson Cavani ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo 3, mchezo wa leo ni wa pili anaukosa kutokana na adhubu hiyo mchezaji mwingine ni Phil Jones.


Na Manchester City watawakosa wachezaji 6 kuelekea kwenye mchezo wa leo kutokana na Covid-19 ambao ni Gabriel Jesus, Kyle Walker, Ederson Moraes, Tommy Doyle, Eric Garcia na Ferran Torres, wachezaji wengine watakao kosekana kutokana na majeruhi ni Nadhani Ake na Aymeric Laporte.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad