Hoteli mbili Zanzibar zateketea kwa moto

Wageni 338 wakiwemo watalii kutoka nchi mbalimbali wamenusurika baada ya hoteli walizofikia ambazo ni  Oceanic Paradise na Toptune Bluu zilizopo Pwani ya bahari ya Hindi  Wilaya ya Kaskazini 'A' Mkoa wa Kaskazini Unguja kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Januari 16, 2021 huku Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Leila Mohamed Mussa akiieleza Mwananchi Digital kuwa hakuna aliyejeruhiwa.

Baadhi ya watalii hao walihamishiwa katika hoteli za jirani kwa ajili ya usalama licha ya awali kutaka kubaki katika hoteli hizo, “licha ya baadhi ya wageni kupenda kubaki hoteli hizo lakini kutokana na athari imeamuliwa wapelekwe hoteli nyengine ambazo zipo katika hali ya usalama.

Leila amesema  katika Hoteli ya Oceanic  kulikuwa na wageni 129  na ile ya Toptune ambayo imeteketea zaidi hasa vyumba ilikuwa na wageni 209.

Huku akikishukuru kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kufanya shughuli yao kwa uhakika na kusaidia kuzima moto kabla ya kuleta athari zaidi, amesema kuteketea kwa hoteli hizo kutaathiri mapato ya Serikali kwa maelezo kuwa zilikuwa zikilipa kodi ya zaidi ya Sh2 bilioni.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad