Virusi vya corona (Covid-19) vimegundulika ndani ya ice cream iliyotengenezwa katika jiji la Tianjin karibu na mji mkuu wa Beijing nchini China.
Mamlaka iliripoti kuwa kampuni ya Vyakula ya Daqiaodao iliyotengeza barafu za ice cream, iliidhinishwa kwa muhuri na wafanyikazi wake walipimwa Covid-19.
Taarifa zaidi zimefahamisha kwamba bidhaa za ice cream zilizogundulika kuwa na virusi zilikamatwa ambapo katoni elfu 29 zilikuwa bado hazijauzwa, na zile zilizouzwa zikakusanywa kutoka kwa wateja.
Serikali ilitangaza kuwa unga wa maziwa yaliyotumika kwenye ice cream ulitoka New Zealand na viungo vingine vilitoka Ukraine.
Serikali ya Beijing ilidai kwamba virusi ambavyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza mjini Wuhan, China mwishoni mwa mwaka 2019, vilisafirishwa kupitia vyakula vilivyoletwa kutoka nje ya nchi.