Katibu wa Idara ya Ulinzi ya Marekani Christopher Miller, alitangaza kuwa idadi ya wanajeshi waliokuwa wakihudumu Iraq na Afghanistan ilipunguzwa hadi 2,500.
Mchakato wa kuondoa wanajeshi kutoka Afghanistan na Iraq ulioanzishwa na Wizara ya Ulinzi (Pentagon) kufuatia agizo la Rais wa Marekani Donald Trump, umekamilika.
Akitoa taarifa juu ya suala hilo, Miller alisema kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ilipunguzwa hadi 2,500, na kubaini idadi ya wanajeshi nchini humo ilifikia kiwango cha chini zaidi tangu mwaka 2001.
Miller alisisitiza kuwa mpango wa Idara ya Ulinzi wa kuondoa wanajeshi wote wa Marekani kutoka nchi ya Afghanistan ifikapo mwezi Mei kama iliyo kwenye makubaliano yaliyofanywa, utategemea na hali nchini.
Miller aliongezea kusema,
"Pande zote lazima zitimize ahadi zao za kuendeleza mchakato wa amani. Isitoshe, Marekani itaendelea kuchukua hatua (za kijeshi) ikiwa itaona umuhimu wa kulinda nchi yetu, watu wetu, na masilahi yetu."
Katika taarifa aliyoitoa kuhusu Iraq, Miller alieleza kuwa idadi ya wanajeshi nchini humo pia ilipunguzwa hadi 2,500 na kusema,
"Uondoaji huu ni unaashiria dalili ya ukuaji kiuwezo kwa vikosi vya usalama vya Iraq."
Miller alimalizia kusema kuwa mchakato huu wa kupunguza wanajeshi unaambatana na mchakato wa mpito wa "Operesheni ya Amani na Utulivu" ilioanzishwa ili kupambana na DAESH, na wala haumaniishi kuna mabadiliko katika sera ya Marekani.
Miller alibaini kwamba wataendelea kuwa na majukwaa muhimu ya kukabiliana na ugaidi na ujasusi nchini Iraq.