Idara ya polisi ya New York yashtakiwa Marekani



Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa New York iliishtaki Idara ya Polisi ya New York (NYPD) kwa matumizi ya nguvu katika maandamano ya Black Lives Matter, yaliyoanzishwa kufuatia kifo cha Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika George Floyd kutokea, baada ya shinikizo za polisi.


Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James, alizungumza na waandishi wa habari na kusema kwamba matumizi ya nguvu ya Idara ya Polisi ya New York (NYPD) sio jambo geni, na hayawezi kukubalika.


Akibaini kupokewa kwa zaidi ya mashtaka 1,300 dhidi ya Idara ya Polisi ya New York tangu Mei mwaka 2020, James alisema kuwa idara ya polisi ilitumia shinikizo za kutisha na harakati za kimabavu kinyume cha sheria, katika maandamano ya amani na kuwazuia mamia ya waandamanaji.


James aliongezea kusema kuwa maafisa walitumia nguvu nyingi kwenye matukio zaidi ya 155, na wakaamua kuchukua hatua ya kuishtaki idara ya polisi.


 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad