Ikiwa Bado Sintofahamu ya CORONA Kuendelea Dunia Wataalam wa WHO Wamewasili China Mji wa Wuhan Kuchunguza Chanzo

Ikiwa Bado Sintofahamu ya CORONA Kuendelea Dunia Wataalam wa WHO Wamewasili China Mji wa Wuhan Kuchunguza Chanzo


 Wakati huohuo wataalamu wa kimataifa waliopewa jukumu la kuchunguza chanzo cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, wamewasili mjini Wuhan nchini China. 

Kuwasili kwao hata hivyo kulicheleweshwa kutokana na kuwepo na msuguano juu ya ziara hiyo. Wataalamu hao watashirikiana na wanasayansi wa China katika kuchunguza, kiini cha virusi vya corona.


 Kirusi hicho ambacho kinasababisha ugonjwa wa COVID-19 kiligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka mmoja uliopita mjini Wuhan. 


China ina wasiwasi wa kunyoshewa kidole juu ya janga la kirusi hicho. Kwa miezi kadhaa mamlaka za China zimeelezea hofu yake ikiwa ni kweli kirusi hicho kilianzia nchini mwake. 


Wanaelezea ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba kuna uwezekano maambukizo ya kwanza pia yaligunduliwa katika nchi zingine. 


Watafiti, kwa upande mwingine wanashuku popo kutoka kusini mwa China kuwa ndio chanzo cha kuenea kwa ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad