Baadhi ya wadau wanasema ni tabia mbaya kuzima simu usiku kwasababu unaweza ukatokea uvamizi nyumba ya jirani na wakashindwa kukupata hewani ukaonekana hauna ushirikiano wakati wa shida
Wengine wanasema, kila jambo na wakati wake. Wakati wa kulala si wakati wa kuhangaika na simu ambayo kutwa nzima umeikodolea macho na kuigusagusa, nayo iache ipumzike. Wanasema taarifa ya msiba, hata ukipewa usiku haikusaidii lazima utasubiri kuche tu
Je, unadhani ni sawa kuzima simu usiku au kuiacha wazi?