Mtoto wa kike wa miezi 11-ambaye alikuwa anakataa kula vyakula vigumu alikuwa kumbe amemeza betri ambayo ilikuwa imekwama kooni kwa kipindi cha miezi minne.
Madaktari walidhani kuwa Sofia-Grace alikuwa na mafindofindo (tonsillitis) au maambukizi ya virusi(viral infection) mpaka alipofanyiwa vipimo vya picha vya X-ray na kubaini kuwa alikuwa na betri ndogo katika koo lake.
Mtoto huyo alifanyia upasuaji wa saa mbili ili kuondoa betri hiyo na sasa anaendelea kula vyakula vya majimaji.
Daktari anasema mtoto huyo amepona kwasababu betri ilikuwa ya zamani na ilikuwa haina nguvu.
Baba yake Calham, kutoka Swindon, aligundua kuwa mtoto wake ana tatizo tangu Januari 2020 na alikuwa anampeleka hospitali kila mara kwa ajili ya matibabu.
Baba yake alikuwa anahisi kuwa kuna kitu kinamsumbua mwanae zaidi ya ugonjwa alokuwa anaambia hospitali, maana alikuwa anakataa vyakula vizito tu.
Safari nyingine alivyoenda hospitali mwezi Mei, alifanyiwa vipimo vya X-ray ambacho kilionesha kuwa mtoto huyo kuwa amemeza betri ambayo inasababisha madhara makubwa katika afya yake.
Bwana Hill alisema : "Alisikitishwa sana alipoiona na alijikasirikia mwenyewe.
Ninajilaumu mwenyewe lakini nimegundua kuwa hakuna kitu ambacho tungeweza kukifanya kujua kuwa amemeza betri.