JPM "Mwambieni Rais wa China Atusamehe Haya Madeni"

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshuhudia Utiliaji wa Saini Wa Mkataba Wa Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa SGR Kutoka Mwanza Kuelekea Isaka, huku akiomba China kusamehe madeni yanayoidai Tanzania likiwemo deni walilolibeba wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR,Rais Magufuli amesema huu ni wakati wa Tanzania na china kujenga uchumi kwa nguvu zote pamoja na kuimarisha ushirikiano.


“Nimemuomba wakatusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa, moja ya deni tunalodaiwa ni  deni tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA lakini kuna deni pia la nyumba za maasakari wetu ambao wamekuwa wapiganaji wazuri dola karibu mil 137 na tushalipa zaidi ya dola 164, na deni la kiwanda cha urafiki dola karibu mil15, hayo nayo nimeomba wakatufutie tu, kwasababu nchi ya china ni rafiki yetu lakini pia ni nchi tajairi na, waziri amesema atalifikisha hili ombi china” amesema Rais Magufuli


Aidha kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje ya China, Wang Yi amesema amefurahia kushuhudia utiaji saini wa ujenzi wa reli ya kisasa, nakusema kuwa wanategemea jitihada anazofanya rais Magufuli katika uboresha na kujengwa miundombinu zitaleta maendeleo kama ilivyo kwenye nchi yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad