Kampuni ya Ndege ya Boeing yakubali Kulipa Dola Bilioni 2.5

 


Kampuni ya ndege ya Marekani Boeing imekubali kulipa fidia ya dola bilioni 2.5 ili kumaliza mzozo wake na wizara ya sheria ya nchi hiyo iliyofanya uchunguzi juu ya ajali mbili za ndege za kampuni hiyo,737 MAX, zilizosababisha vifo vya abiria 346.

Hata hivyo kampuni hiyo imesema haitakubali kulazimishwa kukiri makosa ya uhalifu. 


Wizara ya sheria ya Marekani imesema ufumbuzi uliofikiwa unahusu adhabu ya faini ya dola milioni 243.6, malipo ya dola bilioni 1.77 kwa wateja wa kampuni ya Boeing 737 na kuanzisha mfuko wa dola milioni 500 kwa ajili ya fidia kwa warithi, ndugu na jamaa wa watu waliokufa katika ajali. 


Ajali mbili za ndege za Boeing 737 zilitokea nchini Indonesia mnamo mwaka 2018 na nchini Ethipoia mnamo mwaka 2019 ambapo kwa jumla watu 346 walikufa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad