Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anaamini maamuzi ya Twitter kufungia akaunti ya Rais Donald Trump hayapo sawa kwakuwa uhuru wa Watu kutoa maoni hauwezi kuamuriwa na Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii.
“Uhuru wa kutoa maoni ni muhimu na ni haki ya kila Raia, haki hii inaweza kuingiliwa na Vyombo vya Sheria kama Mahakama sio kwa mitazamo ya Menejimenti za Mitandao ya Kijamii”-Angela
Twitter wameamua kuifungia moja kwa moja account ya Trump ili kuepusha madhara zaidi ambapo kwa sasa yeyote anaejaribu ku-follow account hiyo anaambiwa ‘unajaribu kum-follow Mtumiaji ambae hayupo.
Tukio la juzi la Wafuasi wa Trump kuvamia Bunge la Seneti na kufanya vurugu halikuwapendeza Twitter ambao wanaamini Trump amekiuka kanuni za Mtandao huo kwa kuchochea vurugu hizo