Polisi wamemkamata mwanamume, 20, Abubakar Amodu ambaye alipanga njama na genge moja ya kumteka nyara baba yake na akapokea milioni 2 za Nigeria kama fidia.
Amodu ni miongoni mwa watu 25 waliokamatwa na afisa wa ofisi ya uhusiano mwema katika polisi ya Nigeria, CP Frank Mba, kwa makosa kadhaa waliotekeleza mjini Abuja.
Kijana huyo aliyekamatwa pamoja na wahalifu wengine, alifaya kazi na baba yake ambaye ni mfugaji.
Kijana huyo aliwaambia wanahabari kuwa baba yake alikuwa anafuga ngombe na kwamba alipewa ngombe 15 na akaamua kuondoka nyumbani.
Alitoa ushahidi vile alivyoanza urafiki na genge hilo la wahalifu waliomshauri kumteka nyara baba yake kwasababu hiyo alikuwa njia pekee ya kumuwezesha kutengeneza pesa kwa njia rahisi na kutajirika kwa haraka.
Kijana huyo anakiri kwamba, binafsi alipokea milioni mbili pesa taslim za Nigeria kama fidia iliyotumwa ili baba yake aachiwe huru.