Maafisa kadhaa wamejiuzulu kwenye kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa Rais Donald Trump kufuatia ghasia zilizotokea siku ya Jumatano huko Capitol Hill.
Kufuatia sakata hilo la wafuasi wa Trump kulivamia bunge, washauri wengine wanne kwenye Baraza la Usalama wa Taifa katika Ikulu ya Marekani wamejiuzulu.
Shirika la habari la Reuters limeripoti juu kujiuzulu maafisa hao siku ya Alhamisi ambao ni Erin Walsh, Mkurugenzi mwandamizi wa maswala ya Afrika, Mark Vandroff Mkurugenzi mwandamizi wa sera ya ulinzi, Anthony Rugierro, Mkurugenzi mwandamizi wa maswala ya silaha za maangamizi na Rob Greenway Mkurugenzi mwandamizi wa maswala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Mbali na hao taarifa zinadai kuwa wapo maafisa wengine wanafikiria kuwasilisha maombi yaoya kujiudhulu nyadhifa zao kufuatia matukio hayo ambayo hayajawahi kutokea kwa wafuasi wanaomuunga mkono Trump kuvamia jengo la Capitol wakati Bunge lilipokuwa likianza kuhesabu kura kudhibitisha ushindi wa Rais-mteule Joe Biden.