PAMOJA na Klabu ya Simba kutotaja majina ya makocha waliowasilisha CV zao hadi muda huu, hatimaye imefahamika kuwa jina la kocha mkuu wa zamani wa Al Ahly ya Misri René Weiler limepita hivyo wakati wowote kuanzia leo atatua nchini kuanza kazi.
Simba kwa sasa iko chini ya Kocha Msaidizi Selemani Matola ambaye anakaimu nafasi ya Mbelgiji Sven Vandenbroeck aliyeondoka baada ya kuipekea Simba hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Sven alitua Fah Rabat ya Morocco.
Takriban mwezi unaelekea sasa Simba wamekuwa kwenye usaili wa kupata jina moja la kocha atakayerithi mikoba ya Sven, kufuatia hali hiyo tayari CEO wa Simba, Barbara Gonzalez, amekamilisha mchakato wa kumpata mrithi wake ambaye ni Rene.
Mbali na Rene Weiler, tayari Simba imeshamshusha kocha mpya wa makipa raia wa Brazil, ambapo taarifa zimebainisha kwamba Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo wameshamalizana naye na sasa wamemuachia Barbara jukumu la kocha mkuu ambaye atatua leo.
Chanzo chetu makini kimelieleza Championi Jumamosi kwamba, tayari mchakato wa kuwapata makocha wapya ndani ya Simba umekamilika, ambapo leo Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, inatarajiwa kumpokea kocha Rene Weiler ili aungane rasmi na kocha wa makipa ambaye ni Mbrazil.
“Tayari kazi yetu ya kumtafuta kocha mkuu na kocha wa makipa sisi kama wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi tumeshamaliza, hivyo jukumu lililobaki tumemkabidhi CEO wetu na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usajili, ambapo wao siku ya Jumamosi (leo), watakuwa na kazi ya kumpokea tayari kwa kuingia kambini.
“Kwenye mchakato huo tulipata majina matano, mawili ya kocha wa makipa na matatu kocha mkuu, ila sisi tukampitisha moja kwa moja kocha wa makipa raia wa Brazil, ambaye tayari yupo nchini akimsubiria kocha mkuu ambaye kama haitabadilika atakuwa ni yule aliyekuwa akiinoa Al Ahly msimu uliopita,” kilisema chanzo hicho.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo - Ajira Yako
Championi Jumamosi, baada ya kupata taarifa hizo lilimtafuta Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ili athibitishe taarifa hizo, simu yake haikupokelewa muda wote. MAKOCHA WENGINE Ukiachana na Rene makocha wengine ambao wanaripotiwa kuwa huenda wakatua Simba ni Frolent Ibenge ambaye ni raia wa DR Congo na Steve Kean raia wa Scotland