Kocha Sven ndio basi tena SIMBA, rekodi zake Kiboko


Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imetangaza rasmi kuachana na kocha wake mkuu Sven Vandebroeck kwa makubaliano ya pande mbili.

Kocha Sven Vandenbroeck(Pichani) enzi zake akiwa katika majukumu yake ya kukinoa kikosi cha Simba.

Nafasi ya Sven itakaimiwa kwa muda na kocha msaidizi Seleman Matola mpaka atakapotangazwa kocha mwingine atakayekinoa kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji aliiongoza Simba katika mchezo wake dhidi ya Fc Platinum ya Zimbabwe na kushinda kwa jumla ya bao 4-1 matokeo yaliyowavusha hadi hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika.

TAKWIMU ZA SVEN NDANI YA SIMBA

Mechi-55

Ushindi-39

Sare-10

Vipigo-6

Mataji ya VPL-1

FA-1

Ngao ya Jamii-1

Kocha bora wa mwaka 2020

Makundi ya CAFCL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad