Magufuli "Wivu unavyowakwamisha watanzania"

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amefungua miradi ya maendeleo  Kahama na kutaja wivu kuwa mmoja ya kitu kilichokuwa kinawakwamisha watanzania.



Akizungumza mara baada ya Uwekaji wa jiwe la msingi viwanda vya nafaka maziwa na vinywaji, Kahama Rais Magufuli amepongeza jitihada zilizofanywa na wamiliki wa kiwanda hicho  huku akisema kuwa watanzania tunaweza.


“Nawapongeza sana mmeonyesha watanzania mnaweza sisi watanzania tunaweza , na tunaweza katika hali zote kitu kilichokuwa kinatusumbua sisi watanzania ni wivu, kuoneana wivu na kukwamisha na mimi nataka nione mabillionea wengi wapo Tanzania” amesema Rais Magufuli


Aidha Rais Magufuli ameitaka wizara ya Nishati hadi kufikia mwezi wa saba ambapo kiwanda  hicho kitaanza kufanya kazi sambamba na miradi mingine inayotumia umeme kushughulikia tatizo la ukatikaji wa umeme mara kwa mara .


“Mpaka kufika mwezi wa saba umeme usije ukakatika hata siku moja kukatika kwa umeme ni kuchelewesha maendeleo, ni jukumu la wizara ya nishati kupanga mikakati" amesema Rais Magufuli

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad