No title




MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema inaudhi kupokea ujumbe kwenye simu wa promosheni unaotumwa na kampuni za simu za kiganjani akishauri zingekuwa za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya sheria.

 

Makamu wa Rais ameyasema hayo jana Jumapili, Jnauari 24, 2021 jijini Dodoma katika maadhimisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu.

 

Amesema mitandao ya simu inatuma ujumbe mfupi mwingi wa promosheni ambayo wakati mwingine unakera.

 

“Unapokea ujumbe nyingi sijui kajazwa tena, kajanjaruka tena, natamani niwajibu kuwa usiniudhi, lakini ndiyo ukitumia ujumbe huo hauendi

Ikiwezekana jumbe hizo zitumike kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya kisheria ili waweze kupata haki zao,” amesema Makamu wa Rais.

 

Amesema wananchi wengi hususani wa vijijini, wanashindwa kufikia haki zao za msingi kutokana na ukosefu wa elimu hivyo ni wakati mwafaka wa kutafuta suluhisho la changamoto hiyo.

 

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Frofesa Ibrahim Hamis Juma amesema Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha wiki ya sheria Februari Mosi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad