Mamia ya wakazi wa wilaya ya Buzi nchini Msumbiji wanasubiri kuondolewa katika eneo la kituo cha Guara Guara baada ya nyumba zao kuharibiwa na kimbunga Eloise.
Baadhi ya wakazi waliozungumza na gazeti la nchini humo Noticias wamesema kuwa wamekuwa kwenye msururu siku ya tatu leo.
Taasisi ya kitaifa inayoshughulikia udhibiti wa majanga (INGD) imesema operesheni zimekuwa zikiendelea kwa namna ya kuhakikisha usalama wa kila mmoja.
Baadhi ya wale walioondolewa wamepelekwa kwenye makazi binafsi huku wengine wakipelekwa kwenye vituo vya makazi.
Mkuu wa shirika la INGD Luisa Meque amesema watu wanapaswa kuondoka kutoka kwenye maeneo hatari mapema, Noticias limeripoti.
INGD imesema watu wengi walipuuza tahadhari na wale walioondolewa kwanza walikwenda kituo cha Guara Guara kwa nguvu.Noticias limeripoti.
Familia nyingi zimeendelea kuwasili Guara Guara, na haijulikani itawachukua muda gani kuondolewa.