Hizi ni faida kwa Simba SC na Tanzania baada kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika hapo jana kwa ushindi wa jumla ya magoli 4 – 1 dhidi ya FC Platinum.
Kwakufanya vizuri Simba kwenye mashindano haya ya Klabu Bingwa Afrika itaweza kusaidia kuongeza wingi wa timu za Tanzania ambapo jumla ya timu nne zitapata nafasi kwenye mashindano ya Chama Cha soka Barani Afrika CAF kwa maana ya Klabu Bingwa na Shirikisho.
Kwakuingia hatua hii ya makundi klabu ya Simba SC itajiingizia kitita chs fedha za Kitanzania Tsh Bilioni 1.3 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika CAF wakati ambapo bado fedha kutoka kwa Mdhamini wao Mkuu SportPesa kwa kufanikiwa kutika hatua hiyo.
Simba wanaweza kupata zaidi ya Shilingi Milioni 200 za Kitanzania kutoka kwa Mdhamini wao Mkuu SportPesa kama zikiwa mahususi kwa ajili ya kuipa hamasa timu hiyo.
Mwaka 2019 Kampuni hiyo ya SportPesa ambayo pia ni wadhamini wakuu wa Yanga SC waliwapatia Simba SC kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 50 kwa Simba kuingia hatua ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage kupitia Wasafi Fm amesema kuwa wachezaji walikuwa na morari kubwa kwenye mchezo wa jana hasa kutokana na mashabiki na wanachama wao kuwapa hamasa na ahadi waliyoahidiwa na ‘Management’ ya timu hiyo ya kuwapatia bonasi ya Shilingi Milioni 250 iliyowafanya wachezaji hao kuelewa umuhimu wa mchezo huo dhidi ya FC Platinum.
Katika mchezo huo wa hapo jana Simba iliwasukumuza nje ya mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika FC Platinum kwa jumla ya magoli 4 – 1 na hivyo kujihakikishia kuingia katika hatua hiyo ya makundi.
Waliokuwa mwiba mkali kwenye ngome ya FC Platinum alikuwa ni Erasto Nyoni akifunga goli dakika ya 39, Shomari Kapombe bao lake dakika ya 61, John Bocco na Chama wakifunga kwenye muda wa nyongeza kabla mpira kuisha.