Marekani yailaani Urusi kwa unyanyasaji




Serikali ya Marekani imelaani vikali unyanyasaji dhidi ya waandamanaji na wanahabari nchini Urusi waliokuwa wakiandamana kutaka kuachiwa huru kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kuwa kukandamiza haki ya raia wa Urusi ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza, kukamatwa kwa Navalny na msako dhidi ya waandamanaji uliofuatia, ni dalili za kutia wasiwasi za vikwazo zaidi dhidi ya asasi za kiraia na haki za kimsingi.

Wizara hiyo pia imeitaka Urusi kuwaachia huru watu wote waliozuiliwa kwa kutekeleza haki zao kuachiwa huru mara moja na bila masharti kwa Navalny, kuunga mkono uchunguzi dhidi ya hatua ya kupewa kwake sumu na pia matumizi ya silaha ya kemikali.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Marekani itashirikiana na washirika wake katika utetezi wa haki za binadamu iwe ni Urusi ama kokote zitakapokabiliwa na vitisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad