Mataifa ya Ulaya yatangaza kanuni mpya za usafiri kufuatia COVID-19

 



Ubelgiji, Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya yameweka sheria kali za kuingia katika mataifa yao, zikitaka vipimo zaidi kuchukuliwa na kuongeza muda wa kukaa karantini ikiwa ni katika jitihada za kuzuwia kusambaa zaidi kwa aina mpya ya kirusi cha corona. 

Mataifa hayo pamoja na Ureno na Finland yametangaza kanuni mpya za kuingia nchini mwao. 


Hii ni baada ya mazungumzo marefu ya viongozi wa Umoja wa Ulaya yaliyolenga kupunguza safari zisizo za lazima katika umoja huo ili kuzuia kirusi hicho kipya kinachotokea Uingereza, Afrika Kusini na Brazil kuendelea kusambaa katika umoja huo. 


Kuanzia leo Jumapili mtu yeyote anaeingia katika mataifa ya Ulaya, kutoka nje ya mataifa hayo, inabidi awe na cheti cha kuonesha hajaambukizwa kabla ya kuingia huku umoja huo ukiwa tayari umepiga marufuku watu wote kutoka Uingereza kuingia katika Umoja huo isipokuwa mizigo na watu walio na safari muhimu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad