Mawaziri wa kundi la G7 walaani kukamatwa kwa Navalny



Mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la mataifa tajiri duniani la G7 wamelaani kukamatwa kwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, wakisema kuwekwa kwake kizuizini kumechochewa kisiasa. 
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mawaziri wa Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani imesema kuzuiwa kwa Navalny ni kitendo cha fedheha na wametoa wito kwa mwanasiasa huyo kuachiwa haraka bila ya masharti. 

Mawaziri hao pia wameikumbusha Urusi kuwa ina wajibu wa kitaifa na kimataifa wa kuheshimu na kulinda haki za binadamu ikiwemo za Navalny ambaye yupo kizuizini tangu alipokamatwa Januari 17 

Navalny mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin, alikamatwa muda mchache baada kurejea Urusi kutoka Ujerumani alikopelekwa kwa matibabu kufuatia kisa cha kupewa sumu ya mwezi Agosti mwaka uliopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad