MJI mzito! Mambo kila siku yanaibuka mapya, lile suala la mama yake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ kutamka kuwa baba wa mwanaye huyo siyo Mzee Abdul Juma, limemeibua mazito mengine, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linakupa habari zaidi.
Iko hivi; baada ya mama Diamond au Mondi kutamka vile, Mzee Abdul alijibu mapigo kwa kumtaka Mondi asitumie jina lake.
MATOKEO YAKE…
Matokeo yake ndiyo yaliyotengeneza kichwa cha habari ya leo; inaelezwa kuwa jambo hilo linakwenda kuwagharimu watoto wa Mondi.
Watoto hao si wengine bali ni Naseeb Junior aliyezaa na Mkenya Tanasha Donna, Dyllan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, Tiffah Dangote na Prince Nillan aliozaa na mwanamama tajiri Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
“Yaani ni mazito kwa kweli maana sasa itatakiwa watoto wote hawa wabadili majina ya babu yao, yaende kwa huyo babu yao ambaye ni marehemu Salum Idd Nyange,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya familia ya Mondi.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, Mama Diamond au Mama Dangote hakujua madhara ya jambo hilo na ukubwa wake ndiyo maana aliona ni rahisi tu kutamka, Baba Diamond siyo Mzee Abdul.“Mzee Abdul sasa amechachamaa, anasema hatanii, kweli atakwenda mahakamani kama watalitumia jina hilo kwenye nyaraka zao,” kilisema chanzo hicho.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
UKUBWA WA TATIZO
Chanzo hicho kilitanabaisha kuwa, Diamond au Mondi akishaapa mahakamani na kulikana jina hilo (Abdul Juma), atalazimika kubadilisha pia kwenye hati zake za kusafiria, sambamba na nyaraka nyingine za kampuni, jambo ambalo litakuwa gumu mno.
Kama hiyo haitoshi, kwa watoto ambao wana hati za kusafiria kama vile watoto wa Zari na yule wa Tanasha, watakuwa na kazi hiyo pia ya kubadilisha majina, jambo ambalo linahitaji muda.
MAMA MOBETO ATIA NENO
Baada ya kuwatafuta Tanasha na Zari bila mafanikio, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilifanikiwa kumpata mama mzazi wa Mobeto, Shufaa Rutiginga ambaye alimesema wao kama familia hawaoni sababu ya kumbadilisha jina mtoto wao.
“Sisi hayo mambo yao hayatuhusu, kama wao wameamua hivyo, ni wao na maamuzi yao hayatuhusu. Mtoto ataendelea kutumia jina lilelile la Abdul.
Mtoto wa Mobeto anaitwa Abdul Nasibu Abdul hivyo yeye anatumia jina la babu yake aliyetambulika awali mara mbili kwa maana ya jina la kwanza na la mwisho.
TUJIKUMBUSHEKwa miaka mingi jamii ilikuwa ikiamini baba Diamond ni Mzee Abdul Juma mpaka pale mama Mondi alipokinukisha kupitia Wasafi FM Radio na kusema baba halali wa mwanaye ni Salum Idd Nyange.
WANASHERIA
Hivi karibuni, Gazeti la IJUMAA lilizungumza na baadhi ya wanasheria na wanasaikolojia ili kupata maoni yao kuhusu jambo hili kisheria.“Kwanza inabidi kufahamu baba na Mama Diamond walioana na kama walioana, Diamond amezaliwa ndani ya ndoa? Kama walikuwa mke na mume, mambo yanakuwa tofauti. Kwa sababu hata kama si mtoto wake, kwa mujibu wa vinasaba (DNA) bado kisheria atatambulika kuwa ni mtoto wa Mzee Abdul.“Ila kama siyo mtoto wa ndoa, kinachofanyika ni kumdhalilisha.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
Kwa sababu kama kamlea hadi kufikia kidato cha kwanza, bado anatambulishwa kama mwanaye, anatumia jina lake.“Hilo ni suala la udhalilishaji, hivyo anaweza kuchukua hatua kama kudhalilishwa kwa sababu kama Mzee Abdul angekuwa na uwezo mkubwa kiuchumi sidhani kama angemfanyia hivyo.“
Kosa hilo la udhalilishaji ni sawa na sheria ya madai, ni kwamba anaweza kushtaki mahakamani kudai fidia.“Kiasi cha fidia ni ngumu kutaja kwa sababu Mzee Abdul na mwanasheria wake wanaweza kukaa na kupanga kiasi wanachoona kinafaa,” anasema Mwanasheria Fulgance Massawe kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
“Anayetakiwa kushtakiwa kwanza ni mama, Diamond atafuata kama mshtakiwa wa pili.“Lakini kiujumla hiyo ni sheria ya kudhuriwa kisaikolojia kwa sababu kwanza amemlea mtoto hadi kidato cha kwanza, halafu anakuja kuambiwa si mwanaye.“
Anaweza kudai fidia ambayo itakuwa ni gharama maalum, lakini pia anaweza kudai fidia ya jumla kutokana na madhara aliyoyapata kwa kuambiwa Diamond si mwanaye.“Hapa kuna suala lingine la kupima DNA ili kuhakiki kweli kuwa huyo Mama Diamond alimwekea kanyaboya.
“Hii ni kesi ya madai ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mama na wa pili ni Diamond ili kama kukitokea fidia yoyote ambayo mama anatakiwa kulipa, Diamond awajibike kulipa.“
Kwenye sheria kuna makosa ya madai ambayo hayapo kwenye vifungu vya sheria, kama vile kuzushiwa kesi ya ubakaji ambapo baada ya kufikishwa mahakamani, mahakama ikabaini huna hatia, sasa wewe uliyeshtakiwa unaweza kumshtaki yule aliyekushtaki na kudai fidia kutokana na kukusababishia usumbufu.“
Kesi ya madai haiwezi kumfunga mtu, lakini Diamond anaweza akatakiwa kumlipa Mzee Abdul shilingi milioni 10 kama Mama Diamond hana,” anasema Mwanasheria Joseph Salira.