Mbunifu wa vazi la kitamaduni la India maarufu kama sari afariki dunia



Mbunifu wa vazi la kitamaduni la India Satya Paul, afariki dunia akiwa na umri wa miaka 78. Nyota wengi wa Bollywood wanapendelea kuvaa vazi hilo ambalo huwa na rangi za kung’aa.



Alifungua duka la kwanza la nguo za sari mwaka 1980 na kuweka lebo yake miaka sita baadae.

Paul amefariki Jumatano kutokana na matatizo ya kupooza , alisema mwanae Puneet Nanda.

Kabla ya kifo chake aliweza kuwa nguli wa kubuni sari za suruali, sari zenye mistari ya pundamilia na vidotidoti.

“Nilimuona kuwa mbunifu anayetumia vizuri sanaa ,” mbunifu Kaushik Velendra aliiambia The Guardian. Aliongeza kusema kuwa alikuwa anafanya kazi kama mpakaji rangi.

Mbunifu mwingine alitoa wito kwa shule za ubunifu wa nguo kutumia simulizi ya Paul kuwafundisha wabunifu wa kizazi kipya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad