Mexico inataka ushirikiano wa Biden kumaliza mgogoro wa wahamiaji mpakani




Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, amesema kwamba utawala wa Joe Biden unastahili kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro wa wahamiaji kutoka Mexico wanaishi Marekani. Obrador amesema kwamba amekuwa akipendekeza kwamba raia wa Mexico ambao wamekuwa wakifanya kazi nchini Marekani kwa mda mrefu wanastahili kupewa vibali na kutambuliwa kulingana na sheria. Amesema kwamba hatua kama hiyo inastahili kusaidia mipango iliyopo ya kusaidia mataifa masknini ya Amerika ya kati na kusini mwa Mexico, ambayo raia wake wengi wanaingia Marekani kila mwaka kama wakimbizi. Lopez Obrador ametaka utawala wa Joe Biden kufanya mabadiliko makubwa kwa sera za uhamiaji na amesema kwamba ana matumaini makubwa kwamba rais mpya wa Marekani atasdhughulikia swala hilo kwa haraka sana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad