Mkurugenzi WHO kukutana na Mawaziri wa Afrika



Mawaziri wa Afya na Fedha wa Bara la Afrika wanatarajia kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Dk. Tedros Ghebreyesus, kujadili mgawanyo sawa wa chanjo za Covid-19.


”Nitawaambia kuwa tunafanya kila tuwezalo kufanikisha kuanza kwa utoaji chanjo barani Afrika, kuokoa maisha na kurejesha uchumi, kinachobakia ni dunia inapaswa itekeleza jukumu lake” Dk. Tedros.


Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kuyasihi mataifa tajiri kutoa dozi za ziada za chanjo kwa nchi zilizo masikini.


“Nchi tajiri zilinunua karibu dozi za chanjo ya Covid-19 karibu milioni 800, zinazotosha kuchanja idadi yote ya watu wao kabla ya nchi masikini kuwa na uwezo huo,” Dkt Seth Berkley, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la chanjo, Gavi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad