Mwanamuziki nyota wa pop aliye na umri wa mika 38- anachuana kisiasa na mmoja wa viongozi wa Afrika aliyehudumu muda mrefu madarakani katika uchaguzi wa Uganda unaokabiliwa na ushindani mkali
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
Kampeni zilikumbwa na vurugu ambazo zilisababisha vifo vya watu kadha.
Serikali imeagiza kufungwa kwa mitandao yote ya kijamii.
Rais Museveni anasema hii ni kwa sababu Facebook ilipiga marufuku akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.
Sera ya polisi nchini Ugana inasema maafisa watapanda juu ya majengo marefu mjini Kampala siku ya uchaguzi, baaada ya magari yaliyo na silaha kuanza kuzunguka katika mitaa ya jiji hilo.
Vituo vya kupiga kura vinafunguliwa saa moja kwa saa za Afrika Mashariki (04:00 GMT), lakini matokeo ya uchaguzi hayatarajiwi kutangazwa kabla ya Jumamosi.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Kampeni zilikuwa zimepigwa marufuku katika mji mkuu wa Kampala na katika baadhi ya wilaya.
Upinzani unasema hatua hiyo ilichukuliwa kwasababu ya umaarufu wake lakini serikali inasema ilifikia uamuzi huo ili kudhibiti msambao wa ugonjwa wa Covid-19.