Mwanamuziki Keri Hilson Amtetea Donald Trump Baada ya Account yake ya Twitter Kufungwa

 


Keri Hilson amesimama upande wa Donald Trump mara baada ya mtandao wa twitter pamoja na mitandao mingine duniani kufunga kabisa akaunti zake.


Wiki iliyopita Twitter ilitangaza kuifunga kabisa akaunti akaunti ya Donald Trump kutokana na kuonekana kama anachochea vurugu kwa maneno yake makali wakati huu wa sakata la kushindwa kukubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.


Mwimbaji Keri Hilson aliibuka na kusema kitendo hicho ni Ukandamizaji wa uhuru wa kuongea na ni ishara mbaya kwa dunia kwani, kama tu kiongozi wa taifa kubwa ambalo pia ni mfano wa demokrasia ya kweli, anazimwa kuzungumza, Je kwa wengine itakuwaje?


Hilson aliendelea kwa kusema, hasimami kumtetea Trump, lakini amemtumia kama mfano wa uminywaji wa uhuru wa kuongea. Na alisisitiza kwamba kuna watu wa kawaida na viongozi ambao anawafahamu ambao akaunti zao zinafutwa na jumbe zao kufichwa pale tu wanapozungumza kitu kuhusu Serikali iliyopo madarakani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad