Mzee Abdul: Nitamshitaki Diamond, Tulitoa Mimba ya Kwanza




IKIWA ni saa chache baada ya mama mzazi wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Bi. Sandrah,  kuanika kuwa Mzee Abdul Juma ambaye wengi wanamjua kama baba mzazi wa Diamond, si baba Mzazi wa Diamond kwani wakati wanaingia kwenye mahusiano, tayari mama huyo alikuwa na ujauzito wa mwanamuziki huyo, basi mzee Abdul naye amejibu mapigo.

 

“Sasa hivi inabidi msiniite Baba Diamond, niiteni Mzee Abdul peke yake, kama alivyoongea mama na mimi najibu kwa ufupi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa Baba mlezi, nimepata thawabu hata kama ni ndogo.
 

“Kwa aliyozungumza leo najisikia faraja moyoni mwangu sababu nilikuwa najiuliza, kwa nini nikihitaji kitu nakosa halafu wengine wanapata. Kumbe walikuwa wamekaa na mtoto wake wamepanga mambo yao na leo napata jibu kamili kwamba mimi sio baba mzazi ni baba mlezi.
 

“Kwa hiyo atakuwa Diamopnd Platnumz na siyo Naseeb Abdul, akitumia jina langu nitamshitaki, lakini upande wa Queen Darleen kama yeye atakuwa tayari kubaki na mimi kama baba yake, nipo tayari, Diamond tumeachana asitumie tena jina langu, nitabaki kuwa baba mlezi.

 

“Leo Watanzania wamejua kwa nini nilikuwa sipati misaada kwa sababu siyo mhusika. Lakini alichofeli huyo mama ni jambo moja tu, mimi nimeishi naye tangu mwanzo, akawa mjamzito, nikale mpaka nampeleka hospitali anakwenda kujifungua, nimelea mtoto mpaka tukaja kugombana akiwa form one, lakini leo ametoa kauli kama hizo inaonekana walikaa wakapanga na mtoto wake wafanye hivyo.

 

“Mama Diamond hakuwa na mahusiano mengine, kimsingi mimba ya kwanza tulitoa, mpaka nikauza mkanda wangu wa deki ili tukatoe mimba ile. Baadaye tukafanya tena ndipo akapata ujauzito wa Diamond. Kumbe nilikuwa napigwa picha za kudharirishwa? Na mimi nazungumza kwamba Diamond Platnumz siyo mwanangu, sihusiki naye na sipo kwenye familia yao.

 

“Mtoto hagombaniwi, hata mpaka wa nyumba haugombaniwi, kama sio riziki yako achana nacho, najua kama asingekuwa na pesa yasingetokea haya, pengine kwa sababu anajiona hatokufa, wamenivunjia adabu, kama ni mambo ya kifamilia wangeniita tukayamaliza kumbe ndiyo maana nilikuwa nababaishwa.

 

“Diamond alizaliwa Hospitali ya Amana, nilihusika mwanzo mpaka mwisho, malezi na kila kitu lakini hii ni kiburi tu cha pesa, bahati nzuri Diamond hajawahi kuniosaidia chochote, nina maisha yangu napata kidogo kinanitosha. Wakamwonyeshe kaburi la baba yake basi, kama atamfanya Queen Darleen ni mfanyazi wake sawa tu,” amesema Mzee Abdul.

 

Bi. Sandrah amefunguka hayo leo kupitia kipindi cha MashamSham, kinachoruka kupitia Wasafi FM baada ya kupigiwa simu LIVE kufuatia mahojiano ya Ricardo Momo ambaye ameelezea kuwa ni kaka yake na Diamond kwani wanashea baba mmoja ambaye anaitwa Salum Iddy Nyange (marehemu kwa sasa).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad