Nicki Minaj amemuweka hadharani kwa mara ya kwanza mtoto wake wa Kiume aliyempata miezi michache iliyopita na mumewe Kenny Petty.
Kwenye post hiyo aliyoiweka hapa instagram, Minaj ameandika ujumbe na kumshukuru mwanaye kwa kumchagua kuwa mama yake. Pia amewapongeza Wanawake wote ambao walikuwa wajawazito katika kipindi hiki cha janga la Corona kwa kupitia changamoto nyingi.