Onesmo Justine Afariki Akitoa Maji Kisimani

 


Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 aliyetambulika kwa jina la Onesmo Justine, amefariki dunia wilayani Busega mkoani Simiyu wakati wakifanya kazi ya kutoa maji kisimani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao, amesema tukio hilo limetokea Januari 13 katika kijiji cha Nyashimo wilayani Busega ambapo kijana huyo na wenzake watatu (Mabula Solo, Kafika Tito na Emmanuel chambi) walipewa kazi ya kutoa maji katika kisima kinachopokea maji kutoka Ziwa Victoria chenye urefu wa mita 3.8 kwa kutumia pampu iliyokua juu ya kisima.


Imelezwa kuwa, mara baada ya watu hao kujiridhisha kuwa maji yamepungua kisimani humo waliamua kuingia ndani ya kisima ili kutoa maji yaliyosalia kwa kutumia ndoo zoezi ambalo hawakufanikisha na baadae kuamua kuingiza pampu ndani ya kisima ili kutoa maji hayo.


Wakati wakiendelea na zoezi hilo wakiwa ndani ya kisima moshi uliokua ukitoka katika pampu hiyo ulijaa ndani ya kisima na kusababisha watu hao kukosa hewa safi, ambapo watu waliokua katika eneo hilo waliwaokoa na kuwawahisha kituo cha afya cha Nassa kwa ajili ya matibabu.


Baadae uchunguzi ulibaini kwa Onesmo Justine aliathiriwa vibaya na moshi huo hali iliyolazima kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando mkoani Mwanza ambapo akiwa njiani, majira ya saa 1 jioni Onesmo alifariki dunia.


Aidha waathirika watatu Mabula Solo, Kafika Tito na Emmanuel chambi waliruhusiwa baada ya kupata nafuu wakiwa katika kituo cha afya Nassa.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad