Klabu ya soka ya Arsenal imethibitisha mchezaji Mesut Ozil amejiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, ambayo anakipiga Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Arsenal Edu Gaspar amemshukuru Ozil ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2013 akitokea Real Madrid.
Edu ameongeza kuwa anaishukuru sana timu ya Ozil kwa kuonesha ushirikiano mkubwa wakati wa mazungumzo ya kuvunja mkataba.
Kwa upande wake kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa ilikuwa ni wakati mzuri sana kucheza na Ozil pamoja na kumfundisha, anajivunia sana ubora na ubunifu wake uwanjani.
Ozil ameichezea Arsenal zaidi ya mechi 250, amefunga magoli 44 na kutoa Assist 71. Sasa anakwenda kujiunga na nahodha wa Tanzania na mshambuliaji wa Fenerbahce Mbwana Samatta.
Ujumbe wa Ozil
Thank you, Gunners! #YaGunnersYa pic.twitter.com/lkVI2qHC6X